Header Ads

MWANZA-Bundi atabiri matokeo



Image result for ndege aina ya bundi
Mwanza.
 Ndege aina ya Bundi alionyesha uwezo wake baada ya kutabili matokeo ya sare ya mabao 2-2 kati ya Power Fc dhidi ya Morning Star katika mashindano ya Ndondo Cup yanayoendelea kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
 Katika mchezo huo mashabiki wa Power Fc walitinga uwanjani hapo wakiwa na Bundi huyo aliyetabili matokeo kabla ya mchezo kuanza.
Power ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Deograthias Nyaringa, lakini Morning ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Lick Lick na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila upande ukionekana kuwa na uchu wa kufunga bao,Power ilipata bao la pili kupitia kwa Nyaringa aliyefunga tena la pili dakika ya 68 na kuibuka mchezaji bora na kuondoka na Sh 30,000.
Bao hilo liliwaamsha Morning Star na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Masawe Joseph dakika ya 77.
Wakati mechi hiyo ikiendelea, kivutio zaidi kilikuwa kwa mashabiki wa Power Fc ambao muda wote walikuwa wakicheza na Bundi wao akiwa kwenye ungo.
Mashabiki hao wakiongozwa na mfalme wao, Khatib Msusa ‘Mavugo wa Mavugo’ alisema kuwa wao walifahamu mapema kwani Bundi alikuwa ameshawataarifu kuwa mchezo huo ni sare.
“Huyu rafiki yetu ‘Bundi’ hana matatizo kwa mtu, labda uje kwa shari atakuadhibu..kwenye mchezo huu alituambia mapema kwamba itakuwa sare na sisi tukakubali kwahiyo hapa ni kusubiri mchezo unaofuata.”
Msusa alisema kuwa tayari Bundi huyo ameshaonyesha ishara katika mechi ijao watashinda na kwamba wamejipanga zaidi kushangilia mwanzo mwisho

No comments