Header Ads

Thamani ya facebook yashuka kwa $58bn kufuatia kashfa

Baada ya jalada la Forbes kutoa taarifa ya matajiri  10 duniani huku mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerbag akiwa miongoni mwa matajiri hao ambapo ilimuonesha kupanda kwa utajiri kupitia mtandao huo.
Imekuja kubadilika baada ya  mimiliki huyo Mark Zuckerbag kuomba msamaha kufuatia ukiukaji wa sheria ya data ulioathiri zaidi ya watu milioni 50.
Hata hivyo msamaha huo haukuwazuia wawekezaji kutouza hisa zao huku wengi wakishangazwa ni kiwango gani uharibifu huo utaathiri mtandao huo wa kijamii.

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg
Mwanzilishi wa Mark Zuckerberg- hisa za Facebook zilianguka kufuatia habari mabaya ya data

Mtandao huo wa kijamii ulikabiliwa na hisia kali kutoka kwa wanasiasa , wawekezaji na wateja wake kufuatia kashfa ya data
Matangazo mabaya dhidi ya facebook yaliwafanya watangazaji wengine wa matangazo kusema 'imetosha Imetosha'.
Lakini pia hisa katika mtandao huo wa kijamii zilianguka kutoka $176.80 siku ya Jumatatu hadi kufikia $159.30 siku ya Ijumaa jioni.
Hisa za facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na hivyo basi kuipatia kampuni hiyo thamani ya kibiashara ya $104b.
Kufuatia ukuwaji thabiti na utawala katika matangazo ya kidijitali hisa za facebook zilipanda hadi $190 kufikia Februari mwaka huu.
Brian Wieser mchanganuzi mkuu katika kampuni ya utafiti ya Pivital alisema kuwa alipata matokeo mabaya ya hisa za facebook .
''Nilikuwa nikilenga $152 katika facebook mwaka 2018 na hiyo ilikuwa kabla ya kisa cha kashfa iliotokea wiki hii''.
Bwana Wieser anasema kuwa kushuka kwa bei ya hisa kulionyesha kuwa wawekezaji waliogopa kuongezeka kwa udhibiti mbali na wateja kuondoka katika mtandao huo lakini kulikuwa na hatari chache kwa wamiliki wa matangazo kuondoka facebook.
Watakwenda wapi?, Hargreaves Lansdown , mchanganuzi mkuu Laith Khalaf alisema kwamba wiki iliopita ilikuwa mbaya zaidi katika historia ya facebook.
Progamu ya Facebook skriniMojawapo ya siri na ufanisi wa Facebook , kiwango cha wateja wanaojiunga na facebook kinazidi kuwapendeza wateja wake. La kushangaza ni kwamba ni wembe huohuo unaoinyoa facebook wakati inapopoteza idadi kuu ya watumiaji wake kutokana kashfa hiyo.

Facebook share price
Je Zuckerbag ametoa hakikisho kwa wateja wa Facebook?
Mwanzilishi huyo wa facebook alijaribu kuwahakikishia watumiaji wake , hatua muhimu ya kuzuia hilo kufanyika tena ilichukuliwa miaka kadhaa iliopita.
Hatahivyo mwekezaji wa kampuni ya kiteknolojia Passion Capital Eileen Burbidge ambaye pia yuko katika kundi la washauri la waziri mkuu alisema kuwa facebook ilichukua muda mrefu kuwahakikishia watuamiaji wake na wateja wake.
''Swala kwamba mtandao huo ulichukua siku tano kutoa taarifa ambayo ilionekana kuwa na usawa ulikuwa muda mrefu'' , bi Burbidge alisema. ''Nadhani walinyamaza kwa siku nyingi sana''.
Kampuni hiyo imesema kuwa Facebook ilidharau uharibifu uliofanywa na wateja wake walipogundua kwamba baada ya data yake kutumika kisiasa

JIUNGE NA  PASCHALDLUCA.BLOGSPOT.COM SASA

Jiunge nami kupitia , FACEBOOK,INSTAGRAM  na TWITTER @paschaldlucas  ili kupata habari zote zinazotokea Usikose kujiunga  YOUTUBE  na  kuangalia video zote kali kutoka Mwanza 24 Media





No comments