Header Ads

Zari atua Dar wakati Diamond akiwa Dubai



Dar es Salaam. Wakati mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan maarufu Zari Thebosslady akitua nchini Tanzania jana Ijumaa, taarifa zilizopatikana zimeeleza kuwa mzazi mwenzake mwanamuziki Diamond Platnumz yupo nchini Dubai.
Hata hivyo, mtu wa karibu na mwanadada huyo ameliambia Mwananchi kuwa Zari amewasili nchini akitokea Afrika Kusini kwa ajili ya kuzindua duka jipya la bidhaa za nguo linalojulikana kwa jina la Danube.
"Ninachofahamu amekuja kikazi na atakuwepo hapa, uzinduzi ni leo(Jumamosi). Amekuja kwa ajili ya uzinduzi na si kitu kingine." Kilisema chanzo hicho pasipo kutaka kutaja jina.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana kutoka kwa ofisi ya mwanamuziki Diamond Platnumz, staa huyo alikuwa nchini Marekani kwa wiki nzima na hii jana alikuwa Dubai ambapo wikiendi hii anatarajiwa kuwepo visiwani Zanzibar.

No comments