Header Ads

Zikiwa zimebaki siku 17 kuanza kwa kombe la Dunia Russia Jikumbushe post hii ya Waziri January Makamba akiwawaza Suarez, Harry Kane na Herve Renard



Ni kama  wiki mbili tu sasa zimebaki ili kuanza mashindano makubwa sana ya soka duniani pale nchini Urusi, kwa upande wangu na kumbukumbu zangu ni mwaka 2010  tukio ambalo siwezi kulisahau katika michuano ya kombe la dunia ni namna Ghana walivyoikosa nusu fainali.
Na kupitia mitandao ya kijamii leo nimeona post ya  waziri wa mazingiria Mh. January Makamba akikumbushia dhuluma ya makusudi Luis Suarez aliyowafanyia Ghana ili Uruguay wapite.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh Makamba alikumbushia tukio la Champions League namna Ramos alivyomuumiza Salah, na akahusianisha na namna Suarez alivyofanya ukatili mwingine dhidi ya Waafrika 2010 kwa kudaka mpira makusudi uliokuwa ukienda kambani.
Lakini wakati Makamba akiwaza hivyo, nahodha wa timu ya taifa ya nchini Uingereza Harry Kane naye kuna jambo hatakuja kusahau kamwe, Kane yeye sisi tukimuwaza Suarez bado ila kwake hamsahau Ronaldinho Gaucho.
“Ilikuwa mwaka 2002 nakumbuka nilikuwa mdogo ila siwezi kusahau namna ule mpira Ronaldinho alivyouweka pembeni kwenye goli, bado inaniumiza lakini ile ni kati ya mambo ambayo yalinifanya nitamani sana kucheza kombe la dunia” alisema Harry Kane.
Herve Renard ambaye kwa sasa ni mwalimu katika timu ya taifa ya Morocco naye pia ana jambo ambalo linamuumiza na kamwe hawezi kulisahau katika maisha yake japo lilimfundisha jambo kubwa.
“Ilikuwa mwaka 1982, wakati Ufaransa tumepoteza dhidi ya Ujerumani na tukafungwa kwa penati, nilijawa na uchungu lakini hali ile ilinisaidia sana kuelewa kwamba kwenye mpira kuna nyakati chungu ambazo unapaswa kuvumilia”
Kipi wewe unachokumbuka mashindano ya kombe la Dunia miaka yote?

No comments