JAMAA ALIVOMNG'ATA PAKA MBELE NAIBU SPIKA TULIA ACKSON SIKUKUU YA BULAB...
Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Tulia Ackson jana jumapili Juni 10, 2018 alihitimisha tamasha la ngoma za asili za kabila la Wasukuma Bulabo 2018 katika uwanja wa Kisesa Magu mkoani Mwanza.
Tamasha hilo lilianza jumapili iliyopita Juni 03, 2018 ambapo ngoma mbalimbali za asili zilichuana vikali huku ngoma ya Cecilia Bujora ikibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia zawadi ya ng’ombe mmoja na shilingi elfu hamsini, mshindi wa pili ngoma ya Buyeye Isesa iliyojishindia shilingi laki mbili na mshindi wa tatu ngoma ya Mchomoko iliyojishindia shilingi laki moja.
Mhe.Dkt.Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alitoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kukarabati kituo cha Bujora, shilingi milioni moja kwa ajili ya zawadi kwa machifu wa Usukuma na shilingi laki nne zawadi kwa vikundi vilivyoshiriki ngoma.
Aidha umoja wa Watemi wa Usukuma ulimtunuku Mhe.Dkt.Tulia Ackson cheo cha Mama wa mila na desturi zilizo njema na kumopa jina la Solanyiwa lenye maana ya Mteuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella alisema serikali itaweka mikakati ya kushirikiana na uongozi wa kituo cha Bujora ili kuboresha kituo hicho na kulinda utamaduni wa taifa.
No comments