Header Ads

Hifadhi ya kisiwa cha Saanane-MWANZA



Kisiwa cha Saanane (Saanane Island National Park) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mraba 2.18, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania.
Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania mwaka 1964 ikawa hifadhi kamili mwaka 2013.
Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi wa wanyama na kuelimisha jamii, pamoja na kutoa nafasi kwa wakazi wa Mwanza kupumzika.
Wanyama hao ni pamoja na mbogodigidigitembopofupongoswala palangiripundamiliakimatwiganungunungumamba n.kJina la hifadhi hii lilitokana na muanzilishi wa bustani aitwaye Saanane Chawandi. Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.
Wanayama wakali kama faru na mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachwa huru.
Bustani hii iliachwa kuwa pori la akiba mwaka 1991.
Muonekano wa Ziwa Victoria katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo Mwanza ni kivutio kingine kikubwa.
Hifadhi hii inafikika wakati wowote katika mwaka. Na unaweza kufika kwa kutumia boti ukitokea katika mji wa Mwanza.







KARIBU MWANZA TULINDE HIFADHI ZETU.


No comments