YAJUE MAKUMBUSHO YA WASUKUMA YA BUJORA (BUJORA SUKUMA MUSEUM)
Hifadhi hii ilianzishwa miaka ya 1950 na Padri David Clement kutoka nchini Kanada wa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers).
Malengo yake yalikuwa kuunganisha utamaduni wa Kisukuma na Ukristo, maarufu kama utamadunisho (kwa Kiingereza "inculturation") Kituo hiki cha makumbusho kiko chini ya Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza.
Makumbusho ya wasukuma ya Bujora ni moja ya makumbusho ya mfano nchini Tanzania kutokana na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali zikiwemo Mila,tamaduni na desturi na mgawanyo wa tawala wa kabila hilo katika himaya ya kisukuma katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.Ukifika katika makubusho hayo yaliyopo eneo la Kisesa nje kidogo ya jiji la Mwanza utafurahia utamaduni wa kabila la wasukuma na muundo wa utawala wa kabila hilo na njia ambazo wamekuwa wakitumia kuwafunza vijana wa kiume na wa kike wa kabila hilo zikiwemo sanaa,mila na desturi.
Ndani ya makumbusho hayo utasitaabishwa kuona mbinu zilizokuwa zinatumika kuhesabu na kusoma kwa kabila la kisukuma pamoja na michoro ya ramani ya tawala za kabila hilo na watemi wake.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa tawala za kisukuma zilianza kuimalika na kustawi tangu miaka ya 1505,lakini ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo yamekuwa mstali wa mbele katika kuenzi mila na destuli zao zikiwemo za kuvaa nguo za Rubega,shughuri za ufugaji na utamaduni wa kucheza ngoma za asili zinazoambatana na maonyesho ya mazingaobwe,nyoka,fisi nk na mashindano hayo ya ngoma huwa kwa makundi.
Lakini kubwa zaidi ambalo huwa kivutio kwa watu wengi kwa kabila la wasukuma ni namna ya vijana wa kiume wa kabila la kisukuma wanavyoweza kuoa ,ambapo ni kawaida kuona kundi la vijana zaidi ya 30 wakimfuatilia binti mmoja kwa lengo la kupewa lidhaa ya kufaya naye mazungumzo ya kuoana(Chagulaga) na pindi binti anapotoa mkono na kumpa mmoja wa wavulana vijana wengine hutawanyika kwa kuheshimu maamuzi ya binti baada ya kuvutiwa mvulana anayemtaka.
Niwakati mwafaka kwa makabila yote ya tanzania kuwekeza katika makumbusho ya mila na tamaduni zao kwenye mikoa yao kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Nilifanikiwa kufika mkumbusho ya Bujora na hizi ndizo Baadhi ya maeneo ya utalii ya kiutamaduni wa Kisukuma
KARIBU MWANZA,KARIBU BUJORA
No comments