Header Ads

IJUE ROCK CITY SHOPPING & MALL ILIYOKO MWANZA


Mara zote huwa nasema Mwanza ni moja kati ya miji ya Tanzania ninayoizimia, kuanzia hali ya hewa na kwa kila kitu, sasa kama mapenzi yako ni kutazama movies kwa kwenda Cinema, ukiwa Mwanza siku kadhaa zijazo utakua na nafasi ya kwenda Cinema maana kwa mara ya kwanza zinatengenezwa sehemu za kisasa. Ndani ya shopping mall mpya
Jamani Rock City Mall iliyoko Mwanza haina mfano, iko vizuri mno. Kuna ile super market ya TSN jamani utafikiri uko sijui marekani au ufaransa huduma zao na bidhaa huwezi amini kuwa uko Tanzania. Lipo duka la vito vya thamani nilivyoingia nikajiuliza niko Tanzania au Dubai? hadi mhudumu alivyonisemesha kiswahili ndio nikaamini kuwa niko hapahapa bongo. Usalama wa hali ya juu yaani ukiingia na gari unapewa ki kadi kama ki ATM card yaani gari inalindwa kwa computer.

Watoto nao hawajasahaulika jamani, kuna complex ya kuchezea watoto we acha tu hata mwanao hajui kuogelea siku hiyo atajua. Watoto utadhani kambale wanavyotambaa kwenye maji usiku unaingia huna habari. Wapo wahudumu kila sehemu ya mchezo kuhakikisha usalama wa watoto, yaani mzazi unakaa tu kupunga upepo huhangaiki kukimbizana na mtoto kila bembea, hongera sana. Kweli Dar tuhameni wengine Dodoma wengine Mwanza.

Wakazi wa jiji la Mwanza na kanda ya ziwa wanahimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia kitega uchumi cha Rock City Shopping Mall kinachotajwa kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia biashara za huduma na bidhaa.

Imeelezwa kuwa Uwekezaji zaidi unaoendelea kudhihirika katika kitega uchumi hicho ukitumiwa vyema na wakazi wa kanda ya ziwa utakuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Uwekezaji katika jengo hili umekwishatoa fursa za ajira kwa watu















Benki ya NMB imeendelea kutanua mtandao wa matawi yake nchini ili kuwa karibu zaidi na wateja wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilizindua tawi jipya la NMB Rock City lililopo ndani ya jengo jipya la kibiashara la Rock City jijini Mwanza. Tawi hili linafanya jumla ya matawi ya NMB kwa Mwanza mjini kufikia matano na 28 kwa kanda nzima ya ziwa ni imani ya NMB zinduzi huu unaleta tumaini jipya kwa wateja wa NMB jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. Huduma zinazotolewa na tawi hili.



MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI 2016 YALIFANYIKA ROCK CITY MALL JIJINI MWANZA.

Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi  kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki yaliyofanyika  Agost 26,2016 - Septemba 04,2016 katika uwanja wa ROCK CITY MALL SHOPPING Wengine ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia), kutoka bodi ya Washauri TCCIA.





No comments