Header Ads

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAJIPANGA SUALA YA UTEKAJI WA WATOTO ARUSHA

Image result for MRISHO GAMBO
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema  matukio ya kutekwa watoto katika jiji la Arusha yameipa  wakati mgumu kamati ya ulinzi na usalama mkoa na kujipanga kuhakikisha matukio hayo yanadhibitiwa.

Akizungumza katika msiba wa Mtoto Maureen David Njau (6) aliyeuawa na mtuhumiwa Samson Petro   (18) mkazi wa mkoa wa  Geita  Septemba akiwa   mwenzake Ikram Salim, Gambo amesema ni lazima polisi isambaratishe mtandao wote wa watekaji.

Gambo amesema  tukio la kutekwa watoto bado kwake ni mtihani mkubwa  pamoja na kamati ya usalama mkoa  na imefika wakati   kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake  katika kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Arusha.

"Tunaomba  wananchi watoe ushirikiano wa kutosha katika kuwafichua wahalifu  wa mtandao huo kwani  wapo  mtaani na mnaishi nao na wengi wao mnawafahamu  kwa hiyo naomba ukiona unaishi na mtu ambaye humwelewi mienendo yake uripoti katika vyombo vya ulinzi na usalama ili aweze kufuatiliwa. "amesema Gambo.

Aidha kutokana na tukio  hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema  watajenga vituo viwili vya polisi katika Kata ya Olasiti na Muriet kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili iweze kupunguza uhalifu katika maeneo hayo.

Gambo  amesema kuwa, bahati nzuri  kupatikana kwa mtuhumiwa huyo wa Geita ni juhudi za Jeshi la polisi na kufuatia matukio hayo aliyowafanyia watoto hao naye pia Mungu ameweza kumpatia hicho  alichowafanyia wenzake.

Gambo ,  ametoa milioni 2 za rambirambi katika msiba huo ambapo milioni moja atawapatia wazazi wa Maureen huku nyingine wakipatiwa wazazi wa  Ikram Hassan.

Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Lazaro  kata hiyo ina  wageni wengi, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anakuwa mlinzi wa mwenzake kwani kijana huyo aliyefanya uhalifu huo alikuwa anaishi na watu na kama wangeripoti mapema hatua zingechukuliwa mapema.

Viola amewataka  polisi kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kuendelea kuufichua mtandao huo ili kuwezesha kukomesha matukio hayo yasiendelee kushika kasi kwa mkoa wa Arusha na hata Tanzania kwa ujumla.

Naye diwani wa Kata ya olasiti, Alex Martin amesema kuwa, hali ya uhalifu katika mkoa wa Arusha hivi sasa umeshika kasi Sana ambapo unasababishwa na Watu waovu ambao tunaishi nao katika maeneo yetu na hata wengine wanafahamika lakini hawafichuliwi na matokeo yake ndio hayo.

"Zamani kulikuwa na matukio ya kupotea  ng'ombe na baadaye zinapatikana ila kwa sasa hivi inakuwaje binadamu anapotea na anakutwa maiti ni kitu cha kusikitisha  tunaomba kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake katika kufichua uhalifu miongoni mwetu. "amesema Alex.

Naye wakili  wa  kujitegemea, Albert Msando aliyetoa  milioni moja za rambirambi  amesema  ni wakati sasa wa  kuungana pamoja na kuanzisha kampeni ya kuwalinda watoto wetu kutokana na kukumbwa na matukio mbalimbali  ya kikatili yakiwemo ya ulawiti, ubakaji na mauaji vitendo vinavyofanywa na watu wasiokuwa na hofu yoyote
.

No comments