Header Ads

Korea Kaskazini yafyatua kombora kupitia anga ya Japan

Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido nchini Japan.
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa kombora hilo limefyatuliwa kutoka maeneo ya karibu na mji mkuu wa Pyongyang.
Mwandishi wa BBC mjini Tokyo anasema kuwa kombora hilo lilipita anga za juu zaidi na kwenda mbali zaidi ikilinganishwa na kombora la awali.
Jaribio hilo linakuja siku chache tu baada ya baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani Rex Tillerson ametoa wito kwa China na Urusi kuchukuwa hatua za moja kwa moja dhidi ya Pyongyang, huku waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitaja jaribio hilo la hivi punde kuwa ni kitendo cha kuudhi.
"China huiuzia Korea kaskazini mafuta yake huku Urusi likiwa ndio taifa lililowaajiri raia wengi wa Korea kaskazini.
China na Urusi lazima zionyeshe kwamba zimechoshwa na hatua ya Korea Kaskazini kuendelea kufanyia majaribio makombora yake kwa kuichukulia hatua ya moja kwa moja.
Dakika chache baada ya ufyatuzi huo Korea Kusini ilifyatua makombora mawili ya masafa marefu baharini katika hatua ya kuionya Korea Kaskazini kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Kiongozi Kaskazini Kim Jong-un katika picha hii iliyotolewa na KCNA Pyongyang Septemba 3, 2017.
Korea Kaskazini ilifanyia majaribio bomu la nyuklia mapema mwezi Septemba
Rais Moon Jae-in alifanya kikao cha dharura na kuonya kwamba kombora hilo litasababisha vikwazo zaidiBBC map
 ya Korea kaskazini.
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa jaribio hilo la hivi karibuni, likiwa la kwanza tangu vikwazo dhidi ya Korea kaskazini kuimarishwa wiki iliopita lilifanyika katika eneo la Sunan Kaskazini mwa Pyongyang.
Na kama kombora la hapo awali, hili la sasa pia lilipitia katika anga ya kisiwa cha Japan kilichopo kaskazini mwa taifa hilo cha Hokkaido na kuanguka katika bahari ya pacific

No comments