KARIBU KWENYE BLOGU YANGU INAYOFAMIKA KWA JINA LA PASCHALDLUCA.BLOGSPOT.COM
Pia kupitia mitandao ya kijamii Facebook,Twitter na Instagram kwa jina la Paschaldlucas.
YOUTUBE: DLUCAS TV
Vile vile nifuatilie kwenye Facebook Page Ya MWANZA 24 MEDIA KWA HABARI ZAIDI.
"KAMA IPO, IPO TU."
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 15, 2017 amefanya ziara Kilimanjaro kukagua ukrabati wa magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi DSM ambayo awali yalikaa kwa muda usiopungua miaka mitano bila kufanya kazi. Magari hayo sasa yamekamilika na yanatembea na katika wiki mbili zijazo yatakabidhiwa rasmi kwa ajili ya kuongeza na kuboresha ulinzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kukarabatiwa kwa mfumo kisasa tofauti na awali. RC Makonda ameridhika na muonekano wa sasa wa magari hayo ambayo yatarejea barabarani huku akifanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kununua magari mengine. ”Wako baadhi ya wananchi walibeza hili wazo langu la kuyakarabati magari haya kwa kiwango cha Kimataifa, lakini sasa nafurahi kuona ndoto yangu imekuwa kweli. Ni jambo jema kwa Mkoa wetu.” – RC Makonda.
Magari Mabovu 26 yazidi kumpa Kiki MAKONDA
Reviewed by Unknown
on
September 16, 2017
Rating: 5
No comments