Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki
Mwanamke raia wa Misri ambaye aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki kwenye hospitali moja katika umoja wa falme za kiarabu
Eman Ahmed Abd El Aty alikuwa amepelekwa nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa alikuwa amepunguza uzito kwa kilo 300 kutoka kwa uzito wa kilo 500 lakini akafariki kutokana matatizo mengine ya kiafya.
Taarifa za hospitali zinasema kwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa na ugopnjwa wa moyo na matatizo ya figo.
"Tunatuma rambi rambi na maombi yetu kwa familia," taarifa ya hosptali ilisema.
Bi Abd El Aty amekuwa kwenye hospitali huko Abu Dhabi tangu mwezi Mei baada ya kuhamishiwa huko kufuatia upasuaji aliofanyiwa nchini India.
Kabla ya hajafanyiwa upasuaji familia yake ilisema kuwa hakuwa ameondoka nyumbani kwake kwa miaka 25.
Kutokana na hali kwamba hakuwa ametoka kitandani kwa miaka 25, kulikuwa na hatari kwake kuugua maradhi ya kupumua na ili kusafirishwa madaktari walichukua tahadhari kubwa na kumpa dawa za kuyeyusha damu mwilini.
No comments