Header Ads

Utafiti kipi kinafanyika kwenye ubongo wakati wa kupiga miayo

 
Mara nyingi unapo muona mtu wa karibu anapiga miayo ni lazima nawewe atakuambukiza utapiga miayo hali hiyo imepelekea Watafiti kuchunguza nini kinachofanyika katika ubongo wa binadamu kinacho chochea hali hiyo.
Kupiga miayo mara kwa mara, ni dalili ya echophenomena – yaani namna ya kuiga maneno ya mtu mwingine na matendo bila ya kujijua. Hali hii ya Echophenomena pia inaonekama katika Tourette’s, aidha katika hali ya mtu kuugua kifafa na tawahudi.
Timu ya watafiti katika Chuo kikuu cha Nottingham, imegundua kinachofanyika kwenye sehemu ya mwendo ndani ya ubongo wa binadamu, sehemu ya primary motor cortex pia inatumika pakubwa kwenye hali kama Tourette’s syndrome, yaani kinachofanyika wakati mtu anapopatwa na ugonjwa wa neva.
Ili kufanyia uchunguzi kile kinachofanyika ndani ya ubongo wa mtu wakati wa hali hiyo ya kupiga miayo, wanasayansi waliwachunguza watu 36 waliojitolea, huku wakiwachunguza wengine wakipiga miayo.
‘Excitability’ ni hali ya kuweza kusisimuliwa kufanya kitu sawa na anachofanya mtu mwingine.
Katika utafiti huo, ambao umechapishwa katika jarida la biolojia la Current Biology, baadhi ya waliochunguzwa waliambiwa kuwa ni lazima mtu kupiga miayo, ilihali wengine wakiambiwa kuzuia hali hiyo kufanyika au kukandamiza hamu.
Kwa ujumla, hamu ya kupiga miayo iliamuliwa kuwa ni namna kila motor cortex ya kila mtu inavyofanya kazi

No comments