Uteuzi: Dkt. Shein afanya uteuzi wa viongozi 10 leo
Uteuzi: Dkt. Shein afanya uteuzi wa viongozi 10 leo
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika baadhi ya Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:
- Dkt. Idris Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
- Bwana Joseph Abdulla Meza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
- Bwana Juma Ali Juma ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko
- Bwana Bakari Haji Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar
- Bwana Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko
- Bwana Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango
- Kapteni Khatib Khamis Mwadini ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja
- Bwana Abeid Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete – Pemba
- Bwana Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Pemba
- Bibi Salama Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Pemba
Uteuzi huo umeanza leo Septemba 22, 2017 na wataapishwa siku ya Jumaapili Septemba 24, Saa 2:30 Asubuhi.
No comments