Header Ads

HII HAPA SIRI YA HABARI MAALUM



Afisa Habari wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji cha Habari Maalum Bw.Nehemia Emmanuel Rubondo kilichopo Ngaramtoni Arusha akiwatangazia wanachuo uzinduzi wa wa Studio mpya za Radio na Runinga kuwa utafanyika Novemba 25,2017 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Mrisho Gambo.

Akizungumza chuoni hapo na wanachuo wa chuo hicho alisisitiza kuwa kila mwanachuo anatakiwa kushiriki ili kushuhudia tukio hilo la uzinduaji wa studio hizo.

Aidha uzinduaji wa studio hizo za kisasa kutaongeza ufanisi kwa wanachuo katika kujifunza masomo ya nadharia na vitendo chuoni hapo.

Pamoja na uzinduzi huo wa studio za Radio na Runinga kutaambana na sherehe Mahafali ya wahitimu wa masomo ya uandishi wa habari na utawala kutoka chuo hicho.


No comments