Header Ads

Jeshi la Zimbabwe ladhibiti kituo cha habari cha taifa ZBC

Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Wanajeshi wakiwa na silaha nzito wameoneakana wakirandaranda mjini Harare
Sauti za milipuko mikubwa zimesikika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, ambako inaarifiwa kuwa wanajeshi wamechukua udhibiti kituo cha utangazaji cha taifa ZBC.
Magari ya wanajeshi waliojihami kwa silaha yameonekana maeneo ya mjini Harare.
Hali hiyo ya wasi wasi wa lolote kuweza kutokea, imeanza hapo jana jioni, ambapo wanajeshi wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
Hata hivyo taarifa zinasema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo la utangazaji ZBC, waliambiwa na wanajeshi hao kwamba hawapaswi kuwa na wasiwasi na kwamba uwepo wa vikosi hivyo ni kwa lengo la kulinda eneo hilo.
Milipuko mizito imeendelea kusikika pia.
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe Constantino Chiwenga alitahadharisha uwezekano wa jeshi kuchukua nchi
Chama tawala nchini Zimbabwe kimemtuhumu mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga, kwa hatua yake ya madai kuwa jeshi lipo tayari kuingilia mzozo huo wa kisiasa kwa lengo la kulinda wapigania uhuru wa taifa hilo.
Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na Rais Robert Mugabe kutokana na hali ya sasa nchini mwake.
Marekani imesema kuwa inafuatilia kwa karibu hali ya Zimbabwe na kutoa rai pande zote kutatua mzozo huo kwa njia ya amani
Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe
Naye Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe kupitia ukurasa wake wa Tiwtter amesema kuwa leo watasitisha shughuli za kiofisi ubalozini hapo kutokana na halisi ya sasa mjini Harare.
Balozi wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini Isack Moyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali ipo imara katika jambo hilo na kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mapinduzi.

No comments