Header Ads

Mchungaji atumia pombe kubatiza Waumini Wake


Mchungaji mmoja huko Afrika Kusini amekuwa akikosolewa vikali baada ya kuanza kubatiza washirika kwa kutumia vilevi ambavyo wanavipenda kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu.

Askofu Tsietsi Makiti, (52) ambaye pia  ni Mwanzilishi wa kanisa hilo linalojulikana kama 'Gabola', amesema kuwa ameongozwa na maandiko katika Biblia ambapo Yesu alibadilisha maji kuwa divai.

"Watu wanao kunywa na kubatizwa na bia wana furaha na amani. Hii inamaanisha kuwa wanaishi katika kivuli cha Mungu, "alisema Makiti.

Kanisa hilo lenye jina 'Gabola'  likimaanisha 'Kunywa' limesema linakubali kuwapokea waumini waliotoka makanisa mengine huku likiweka wazi kwamba idadi ya watu wameongezeka kufikia 500 ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.

Waumini pia wanaruhusiwa kunywa wakati huduma za kanisa zikiendelea.

Aidha Askofu huyo ameweka wazi kwamba ana mipango ya kuanzisha matawi ya kanisa lake hilo katika miji mbali mbali.

Source: Mwananchi

No comments