Header Ads

RAIS MH.DKT JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MSEVEN WA UGANDA KWENYE IKULU YA MASAKA

Nimekusogezea picha zote za matukio ya Mazungumzo kati ya Rais  Mh.Dkt.John Pombe Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Mseveni wa Uganda.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini UgandaRais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la mkutano baina ya wajumbe wa nchi mbili za Tanzania na Uganda katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja aliombatana nao katika Mazungumzo na ujumbe wa Uganda uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za Asili cha Cranes Performance mara baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini UgandaKikundi Cranes performance kikitumbuiza katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Masaka Uganda. PICHA NA IKULUSource: IssaMichuSource; Issa Michuzi

No comments