Header Ads

WATOTO 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO BILA KUFUNGUA KIFUA

WATOTO 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO BILA KUFUNGUA KIFUA. Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) ya nchini Israel wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 20 wenye matatizo ya Moyo.Upasuaji huo ambao unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 23/11/2017 na kumalizika kesho tarehe 27/11/2017. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuziba matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo.Katika kambi hii tunatarajia kufanya uchunguzi wa moyo kwa watoto 100 kati ya hao watoto 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na watoto 40 watatibiwa hapa nchini.Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 25 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 20 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri.

No comments