Header Ads

AJALI KAGERA YAUA NA KUJERUHI WATU



Kutoka Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera basi  la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake kati ya Kaisho, Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha kifo cha kondakta wa basi hilo.

Kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali teule ya Nyakahanga na wengine katika Kituo cha Afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali. 

Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyotolewa juu ya majeruhi wa ajali hiyo

No comments