Header Ads

Mkuu wa Wilaya ampongeza Mumewe kwa Kuongeza Mke



Katika hali ya kawaida kwa mwanamke sio rahisi sana kumruhusu mme wake kuongeza mme na inawezekana ikaonekana ajabu kwa wengi kutokana na ugumu wa Wanawake wengi kukubaliana na sheria ya Dini ya Kiislam ya mume kuruhusiwa kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini hilo limekuwa jepesi kwa mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah baada ya kumruhusu, kumuandaa na kumpongeza mumewe kwa kuengeza mke wa pili.
Bi. Zainab Abdallah ambaye anatajwa kama Mkuu wa Wilaya Mdogo kabisa kwasasa hapa Tanzania ni Mke halali wa Abdul Muhammed ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam nawalifunga ndoa takribani miezi 7 iliyopita.
Mkuu wa wilaya huyo amezitoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram kwa kuandika na kuweka picha ya Bi Harusi na Mumewe baada ya kufunga ndoa

No comments