Header Ads

POLISI YAKIRI KUMPIGA RISASI MWANAFUNZI WA NIT

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Lazaro Mambosasa amekiri kwamba mtu mmoja alipigwa risasi na Polisi hapo jana. Mambosasa amedai kwamba Polisi walikuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana ndipo walipiga risasi juu na moja kati ya risasi hizo ilimpata mtu.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi inakuja katika wakati ambapo simanzi imetawala mitandao ya kijamii kutokana na taarifa za binti Aquilina anayetajwa kupigwa risasi na Polisi hapo jana maeneo ya Kinondoni Mkwajuni wakati Polisi wakikabiliana na wafuasi wa Chadema

No comments