Header Ads

Arnold Schwarzenegger afanyiwa upasuaji wa moyo

Kutoka Marekani mcheza filamu na mwigizaji maarufu wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao umemalizika salama usalimini.

Arnold Schwarzenegger ambae amecheza katika  takriban filamu 50 na kabla ya kuwa gavana wa Jimbo la California 


Akithibitisha kuhusu upasuaji huo meneja wa nyota huyo amesema kuwa mnamo mwaka 1997 Arnold Schwarzenegger aliwekewa "pulmonary valve",na upasuaji huu umefanywa ili kumuwekea "pulmonary valve" mpya.

Kama kawaida katika filamu zake Schwarzenegger hutumia sana neno la "I'll be back"na baada ya upasuaji amerekodiwa akisema, "I am back".

Arnold Schwarzenegger, ambaye alianza kujenga mwili wakati wa umri wa miaka 15.

Ikumbukwe Arnold Schwarzenegger alishawahi kushinda tuzo ya Mr.Universe akiwa na umri wa miaka 20.



Usipitwe!! Jiunge nami kupitia FacebookTwitter na Instagram kwa jina @paschaldlucas ili kupata habari zote na matukio ya kila siku, Pia usikose kujiunga (Kusubscribe)nami kupitia Youtube kuangalia video kupitia DLucas Tv
Kwa kunitumia stori nitumie kwa simu namba 0762 006 415, E-mail: paschald.lucas@gmail.com

No comments