Header Ads

KATIBU WA BUNGE STEVEN KIGAIGAI AZUNGUMZIA AJALI YA WABUNGE MOROGORO

Baada ya kutokea kwa ajali ya wabunge sita usiku, Machi 29, 2018 mkoani Morogoro katibu wa Bunge, Steven Kagaigai amesema chombo hicho cha dola kinafuatilia kwa ukaribu kuhusiana na ajali ya wabunge hao.

Kagaigai ameeleza kuwa  baada ya kupokea taarifa hizo za ajali wamefanya mawasiliano na uongozi wa Hospitali ya Morogoro na walishauriwa kuwahamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

“Ndiyo taarifa hizo ninazo, wamepata ajali huko Morogoro, tayari tumeshafanya taratibu za kuwapeleka Muhimbili kwa huduma zaidi na ofisi yetu inawajibika kwa kila hatua,” alisema Kagaigai.

Majina ya wabunge hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).


Usipitwe!! Jiunge nami kupitia FacebookTwitter na Instagram kwa jina @paschaldlucas ili kupata habari zote na matukio ya kila siku, Pia usikose kujiunga (Kusubscribe)nami kupitia Youtube kuangalia video kupitia DLucas TvKwa kunitumia stori nitumie kwa simu namba 0762 006 415, E-mail: paschald.lucas@gmail.com

No comments