Header Ads

MCHUNGAJI AKAMATWA MOSHI

Mchungaji Fredy Njama wa Usharika wa Karanga, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Moshi mkoani Kilimanjaro amekamatwa na jeshi la Polisi kwa kinachoidaiwa kuwa ni “Uchochezi wa kisiasa”.Mchungaji huyo wiki mbili zilizopita alisoma ripoti katika mkutano mkuu wa mwaka wa usharika wake ambayo ndo imepelekea kukamatwa kwake.Katika ripoti hiyo, alibainisha kuwa mapato ya usharika yanapungua kwa sababu mbalimbaliKatika utangulizi wa ripoti alitaja changamoto 6 zinazoikabili nchi kwa sasa:

Ukosefu wa ajira kwa vijana, Hali ya uchumi inayoyumba, Hali ya kisiasa ni ya mashaka, Gharama kubwa za matibabu, Sera ya elimu bure na Wastaafu kutolipwa mafao yao.

Ripoti hiyo pia imechapwa katik kijitabu na kiwanda cha uchapaji cha Dayosisi hiyoKundi la Polisi na maafisa usalama walimchukua Ijumaa asubuhi hadi kiwandani na kumtaka akusanye vijitabu vyote hadi vilivyosambazwa na kuvikabidhi Polisi.
Aidha walimtaka aandike barua kuomba radhi na kufuta ripoti hiyoJioni ya leo, Polisi walifika ofisi ya usharika na kufanya upekuzi. Walichukua laptop na flash. Kisha walimpakia mchungaji katika gari lao na kuondoka naye.

No comments