RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI WA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI (TAEC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dodoma.
Taarifa iliyotolewa jana March 23 , 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kitivo cha Taaluma na Utafiti.Rais Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine (SUA).Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
No comments