Header Ads

WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII VIBAYA WAPEWA ONYO

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewaonya wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kufanya uhalifu pamoja na kuhamasisha maandamano yasiyo halali kwani kitendo hicho ni kosa kisheria.

Onyo hilo kali  limetolewa jana jumamosi Machi 24, 2018 mbele ya askari   na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina, Ahmed Msangi wakati alipokuwa akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi  yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini jijini Mwanza

Tokeo la picha la Ahmed Msangi

Nafikiri wote sasa hivi mnafahamu kuna hii mitandao ya kijamii kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu, na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa, na kiukweli umepigwa marufuku,
Kuna watu wanafanya fanya hayo kushawishiana, tufanye upelelezi, tuchunguze. Yeyote atayefanya hayo kushawishi tukimng’amua tuweze kumkamata. Tumkamate na tuweze kumhoji wana sababu na nia gani? alisema Kamanda Msangi.


Hata hivyo, Kamanda Ahmed Msangi amewaasa wananchi wanaotumia mitandao hiyo vibaya kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na ni kosa la kimtandao kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kauli hiyo inakuja katika kipindi ambacho kwenye mitandao ya kijamii kuna taarifa za watu kuhamasishana  kupanga maandamano kupitia mitandao ya kijamii kwa  siku zijazo mbele suala ambalo serikali imesema maandamano hayo hayapo katika utaratibu na pia yapo kinyume na sheria za nchi ya Tanzania.

JIUNGE NA  PASCHALDLUCA.BLOGSPOT.COM SASA


 Jiunge nami kupitia FACEBOOK,INSTAGRAM  na TWITTER @paschaldlucas  ili kupata habari zote zinazotokea Usikose kujiunga  YOUTUBE  na  kuangalia video zote kali kutoka Mwanza 24 Media

No comments