Header Ads

VIDEO: WAZIRI MWIGULU NCHEMBA ATOA SABABU ZA KUZUIA MAANDAMANO



WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa wanazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane  na kuharibu taswira ya nchi.
Akizungumza jana katika harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, alisema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.
‘’Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuvuruge,’’ alisema Dk Mwigulu.
JIONEE VIDEO HAPA CHINI

No comments