Header Ads

VIDEO: AJALI MBAYA ILIYOTOKEA LEO USIKU IGUNGA., BASI LA CITY BOY

Basi la kampuni ya City boy linalofanya safari zake kati ya Karagwe na Dar Es Salaam usiku wa leo April 4,2018 limepata ajali  ambapo watu 12 wapoteza maisha na wengine 46 kujeruhiwa katika eneo la Makomero wilayani Igunga, mkoani Tabora.



Akithibitisha na kutoa taarifa za awali za kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora SACP Willprod Mtafungwa amesema ajali hiyo imetokana na basi hilo kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Fuso  lililokuwa linatokea Singida  hivyo basi hilo likaacha njia na kupinduka.



Mtafutwa amesema  kuwa mbali na kuua pia abiria wengine wawili kati ya 46 hali zao sio nzuri wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi

Majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Igunga.



Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku na dereva wa lori hilo kukimbia kusikojulikana hivyo jeshi la polisi linafanya juhudi za kumtafuta dereva wa lori hilo.

Na taarifa kamili toka jeshi la Polisi litatoa asubuhi.

SUBSCRIBE NAMI NA UJIONEE VIDEO HAPA CHINI










No comments