Header Ads

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA SUA MOROGORO, WANACHUO WATOA KERO ZAO

Kutoka Morogoro Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wametoa ya moyoni mbele ya Rais John Magufuli kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwamo uhaba wa mabweni ya wanafunzi na fedha za mikopo

Wametoa ya moyoni baada ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoa nafasi kwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kueleza mambo mbalimbali wanayokabiliana nayo baada ya kufanya ziara katika chuo hicho kilichopo mjini Morogoro

Lakini kabla ya Rais kutoa nafasi hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alieleza mafanikio na juhudi zinazoendelea kufanywa na wizara yake ikiwa ni pamoja na kufanikisha utoaji wa mikopo.

Emmanuel Gwalaje, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya wanyama amesema wapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo hawajalipwa fedha katika muhula wa kwanza na wanaishi maisha magumu hadi sasa chuoni hapo.

Kwa upande wake Mhadhiri wa chuo hicho, God Swai amesema wanafunzi wanaporwa mitaani na kukabwa kutokana na uhaba wa majengo ya bweni, huku akiomba kujengwa kwa ofisi za wahadhiri chuoni hapo.

Mbali na maombi ya wanafunzi, vile vile kulikuwa na maombi ya watumishi, huku Amina Juma akimuomba Rais Magufuli kuwafikiria watumishi wa darasa la saba waliofukuzwa kazi.

Amina Juma amedai kuwa yeye ni mtumishi chuoni hapo tangu mwaka 1994, aliyeathirika na kuondolewa kwa watumishi wa darasa la saba, akiomba wafikiliwe upya kutokana na hali ngumu ya maisha mtaani na kupelekea kukosa mahitaji na mahitaji yao ya kujikimu kutokana na kuwa nje na kazi walizokuwa wakizifanya.

No comments