Header Ads

VIDEO:MWANZA WALIVYOZINDUA PASPOTI ZA KIELEKTRONIKI





Katika kuendeleza kutoa huduma za kijamii  serikali kupitia idara ya uhamiaji imezindua
mfumo mpya wa kutoa pasipoti za kusafiria za kielektroniki  za afrika mashariki mkoa  Mwanza.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.John
Mongella  ambaye pia alikuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi huo amesema kuwa kwa kuwa dunia ya sasa inaenda kielektroniki
na kidijitali kwa hiyo kupitia Pasipoti taarifa zote za mmiliki na mwombaji
zitatunzwa kwa kuwa pasipoti hizi zimewekewa vigezo ambavyo vitasaidia kulinda
usalama na kutunza taarifa za mmiliki.


Hivyo mwombaji ukifanikiwa kukidhi kujaza fomu ya
maelekezo maana yake serikali itakuwa na taarifa zake zote lakini cha msingi na
muhimu ni kuwa na kitambulisho cha taifa kwanza kabla hujaanza kujaza fomu ya
maombi.

No comments