Aung Suu Kyi kutoa hutuba yake kitaifa
Kiongozi wa Myanmar Aung Sang Suu Kyi anatarajiwa kutoa hotuba yake ya kwanza kitaifa kuzungumzia ghasia zinazotokea nchini humo zilizosababisha zaidi ya watu laki nne, Waislamu wa Rohingya, kukimbilia nchini Bangladesh, wiki chache zilizopita.
Aung Suu Kyi ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amekuwa akishinikizwa kimataifa kutoa tamko lake juu ya jeshi la nchi yake, ambalo linatuhumiwa kuwaua na kuwatesa watu hao.
Mataifa ya nchi za magharibi na Umoja wa Mataifa umeitaka Myanmar kumaliza dhulma hiyo na kuwaruhusu wakimbizi hao kurejea nchini mwao.
Mwandishi wa BBC, nchini Myanmar amesema kuwa iwapo Aung Sang Suu Kyi atalikosoa jeshi la nchi yake, jambo hilo litatishia utulivu uliopo katika serikali yake ya kiraia.
Lakini pia asipofanya hivyo, sifa zake alizozipata kimataifa zitapotea.
No comments