Header Ads

Jaji Mihayo Rais wa MCT



Image result for JAJI MIHAYO

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limemchagua kwa mara nyingine  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  kuwa Rais  wake   kwa kipindi cha  miaka mitatu ijayo.
Jaji mstaafu Mihayo amekitetea kiti chake hicho leo huku akiwa hana  mshindani na kuibuka na ushindi wa kura 59 za ndiyo   na mbili za hapana  katika uchaguzi huo uliowashirikisha  wajumbe 61 wa  baraza hilo jijini Dar es Salaam.
Akitangaza matokeo hayo, Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Deogratias Nsokolo amewataja wengine waliochaguliwa kuwa ni wajumbe wa bodi akiwamo   Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Lts (MCL) Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Eda Sanga, Dinna Chahali na Wallance Maugo.
Amesema nafasi ya uwakilishi wa wananchi kwenye baraza hilo, aliyechaguliwa ni Jaji Mstaafu Juxon Mlay, Anna Hengan na Edmund Mdolwa.
Pia baraza hilo limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya udhalilishaji dhidi yao.

No comments