Kujichubua kuna madhara kwa ngozi yako.
Na Paschal D.Lucas
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi ng’aavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.
ambapo baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huonekana wapo chini ya kiwango, na hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au chochote kile kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonesha wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika jamii na hata matangazo yenye kushajihisha vijana kutumia vipodozi hivyo vibaya yanaoneshwa kwenye televisheni na sehemu nyengine mbalimbali huonesha kitu hiki.
hali ambayo huzalisha mawazo kwa vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge bila kujali
Madhara ya kujichubua ni yepi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.
No comments