Header Ads

MAKUMBUSHO YA BINADAMU KUZINDULIWA

Image result for makamu wa rais tanzania
Arusha. Makamu wa Rais Samia Suluhu anatarajiwa kufungua  makumbusho ya chimbuko la mwanadamu, katika eneo la Olduvai ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA).
Uzinduzi huo, unatarajiwa kuhudhuriwa na watafiti wa kimataifa wa chimbuko la mwanadamu,mabalozi wa  nchi mbalimbali na watalii wa ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema, makumbusho hayo yatafunguliwa Octoba 3  ambayo yatakwenda sambamba na onyesho la chimbuko la binaadamu.
Amesema  siku ya uzinduzi, utatolewa ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizogunduliwa eneo la Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dk Mary Leakey , Nyayo za zamadamu aliyetembea kwa miguu miwili mika milioni 3.6 iliyopita.

"Pia kutakuwa na maonyesho ya zamadamu na masalia yao walioshi miaka  milioni mbili  iliyopita na na  kutakuwa na historia ya maisha ya jamii inayofanana na binaadamu iliyoishi miaka 1.7 milioni iliyopita na historia ya kipindi cha mwanzo wa binaadamu miaka 200,000 iliyopita"amesema
Akizugumzia makumbusho hayo, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Dk Fred Manongi amesema  yamejengwa  kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania kupitia NCAA na Jumuiya ya Ulaya.

“Makumbusho haya yatasaidia  kuvuta watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani, ambao watataka kujua historia ya mwanadamu, kwani hapa sasa ndio kitovu chache”amesema
Meneja wa Idara ya Urithi wa tamaduni,Mhandisi Joseph Mwankunda amesema ujenzi wa eneo hilo la makumbusho na miundo mbinu yake vimegharimu   Sh 1.7bilioni
Amesema katika makumbusho hayo kutakuwa na eneo la makumbusho, eneo la wafanyabiashara wa zana za asili nakitamaduni na kutakuwa na eneo la chakula na mapumziko kwa watalii.

No comments