Manchester United wamfanya Louis Van Gaal kujuta
Mwaka 2016 wakati Manchester United wakibeba kombe la FA ilionekana wazi kwamba kocha Louis Van Gaal huenda angeendelea kuiona klabu hiyo lakini tofauti na matazamio ya wengi Van Gal aliondolewa Manchester United.
Toka wakati huo kocha huyu amekuwa mkimya na hakuwahi kueleza lolote kuhusu kufukuzwa kwake na Manchester United lakini sasa inaonekana LvG amechoka na ameamua kufunguka yaliyo moyoni mwake.
Ni USALITI, hiyo ndio tafsiri sahihi ya alichosema Louis Van Gaal kwani Mholanzi huyo anadai Manchester United pamoja na CEO wao Ed Woodward walimzunguka wakati wa kufanya maamuzi ndipo wakaamua kumpa nafasi Jose Mourinho.
“Nilikuwa napata presha kubwa na nilijua bodi iko na mimi lakini kumbe walikuwa wananizunguka, mke wangu Truus aliliona hilo mda akaniambia lakini mimi sikuliona na niliona kila kitu kipo sawa kumbe sivyo” alisema Van Gaal.
Van Gaal anasema kuanzia January ya kipindi anatimuliwa mambo yalibadilika na baada ya Jose Mourinho kutimuliwa Chelsea alizidi kuwa kwenye presha kubwa huku mbaya zaidi wachezaji wa zamani wa Manchester United nao wakaanza kumnyooshea kidole.
“Wachezaji wa zamani nao wakaanza kuongea na kufukuzwa kwa Jose kukawafanya wavutiwe zaidi na mimi kuondolewa United, nikijua kuhusu Mourinho kuhitajika United lakini bado niliamini nitapewa muda” alisema LVG.
Van Gaal anasema kati ya vitu viliwahi kumuuma na kujuta kwenye maisha yake baasi ni kufichwa kuhusu ujio wa Mourinho na baadaye mabosi kumuambia baada ya kuona taarifa za suala hilo zimeshavuja.
Louis Van Gaal alipewa Manchester United akirithi mikoba ya David Moyes lakini baadaye naye mwaka 2016 alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho ambaye naye alitoka kutimuliwa Chelsea

No comments