MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2017
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha inategemea kupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 tarehe 03.09.2017 katika eneo la Ofisi ya Kata ya Oldonyowas saa 02:00 asubuhi ukitokea Halmashuri ya Wilaya ya ...
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha inategemea kupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 tarehe 03.09.2017 katika eneo la Ofisi ya Kata ya Oldonyowas saa 02:00 asubuhi ukitokea Halmashuri ya Wilaya ya Longido. Kauli ya Mwenge wa Uhuru 2017 : ”Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya nchi Yetu’.
Katika halmashuri ya Arusha Mwenge wa Uhuru 2017 utakimbizwa umbali wa Kilomita 88 katika kata 7 na kupitia jumla ya Miradi 7 iliyogusa sekta za Elimu, Afya, Maji, Viwanda na Uvuvi yenye thamani ya Tsh. 1,635,900,399.45 fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali ikiwa kiasi cha Tsh.163,350,700.00 ni Nguvu za wananchi, Tsh. 80,849,699.45 Mapato ya Ndani ya Halmashauri,fedha kutoka Serikalini kiasi cha Tsh. 255,000,000.00 pamoja na Michango ya Wadau wa Maendeleo Tsh. 1,136,700,000.00.
Hata hivyo pamoja na kupitia Miradi ya Maendeleo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 kitaifa Ndugu Amour Hamad Amouratakabidhi Hundi za Mikopo zenye thamani ya Tsh. 100,000,000.00 kwa Vikundi 23, Vikundi 16 ni vya Wanawake na vikundi 7 vya Vijana.
Baada ya kukabidhi Hundi hizo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti atasoma Risala ya Utii kwa Mheshimwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na baadaye kuendelea na shughuli nyingine.
Picha Na; PASCHAL D.LUCAS
Toka; CHUO CHA UANDISHI WA HABARI CHA AFRIKA MASHARIKI-ARUSHA.
No comments