Trump autaka U/Mataifa utumie uwezo wake
Umoja wa Mataifa hautekelezi majukumu yake kulingana na uwezo wake ,amesema rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa .
" Uwalenge watu zaidi , urasimu kidogo," alitoa wito huo katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York, akirejelea wito wake wa kufanyika kwa mageuzi.
Hakuna taifa linalopaswa kuwajibika na utofauti wa gharama zinazopaswa kuchangiwa na kila taifa, amesema Trump
Marekani hulipa asilimia 28.5% ya gharama zote za walinda amani, jambo ambalo Trump anasema si la haki.
Wakati alipokuwa mgombea wa urais wa Marekani, Bwana Trump aliukosoa vikali Umoja wa Mataifa, akizungumzia "mapungufu yake na kutokuwa na uwezo".
" haujafikia uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwasababu ya urasimu na utendaji mbaya ,"alisema katika hotuba yake ya uzinduzi.
Amezitaka nchi wanachama "kuchukua msimamo thabiti " wa kubadili utendaji uliozoweleka wa Umoja wa mataifa badala ya " kuendelea kutumia njia zilizopitwa na wakati ambazo kwa sasa hazifanyi kazi ".
Amemtolea wito katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa , António Guterres, afanye mabadiliko.
No comments