UFAFANUZI: Polisi kuhusu kumshikilia Hashim Rungwe
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo September 6, 2017 limetoa ufafanuzi kuhusu ishu iliyokuwa inasambaa mitandaoni kuwa aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe amekamatwa.
Jeshi hilo limesema kuwa kweli linamshikilia Hashim Rungwe ambaye alikamatwa tangu August 28, 2017 akituhumiwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.
Hashim Rungwe anadaiwa kuhusika katika utapeli wa Dola za Kimarekani 30,800 ambazo ni sawa na Tsh Milioni 73 kwa nyakati tofauti akiwa kama Wakili anayeendesha biashara kati ya raia wa Uturuki Ally Riza Bilgen na Kampuni ya Les Tropiques Group Mining SPRL Limited.
Inaelezwa kuwa raia huyo wa Uturuki alikuja Tanzania kwa lengo la kununua korosho tani 15 na kuandikishana mkataba wa malipo ya Dola 72,000 kama gharama za bidhaa hiyo na usafirishaji lakini tangu wamesainishana mkataba huo November 2016, hakuna kilichofanyika na malipo hayo ya awali yalifanywa kwenye akaunti ya Rungwe katika Bank ya CRDB.
No comments