Wabunge waombwa kutokukaa Baa.
Spika Ndugai leo amewausia wabunge wanzake kuwa makini na usalama wao kwa kuchukua hatua zaidi za kujilinda, ikiwemo kutokaa baa mpaka usiku wa manane ili kujiepusha na matatizo mbali mbali yatakayoathiri usalama wao.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo bungeni na kuwataka wabunge kutojiachia sana wanapokuwa sehemu mbali mbali, na wachukue hatua za kuwa makini na maisha yao.
"Waheshimiwa wabunge niwaase tu kuhusu usalama wetu, kwamba tuwe makini na usalama wa maisha yetu na tusjiachie sana tuwapo katika majimbo yetu ama mahala pengine tunapoenda, na tusikae kwenye mabaa hadi usiku wa manane...maana usalama unaanza na wewe mwenyewe", amesema Spika Ndugai
Hivi karibuni mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana, na mpaka sasa yuko nchini Kenya akipatiwa matibabu.
No comments