Wakimbizi 18 wa Burundi wauawa DR Congo
Maafisa wanasema kuwa takriban wakimbizi 18 wa Burundi wameuawa na vikosi vya usalama mashariki mwa taifa la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo .
Wengi wengine wamejeruhiwa.
Maafisa wa DR Congo pamoja na wanajeshi wanadaiwa kuwafyatulia risasi wakimbizi hao walipokuwa wakifanya maandamano ya kupinga mpango wa kuwarudisha nyumbani.
Makumi la maelfu ya raia wa Burundi walitoroka taifa hilo wakati za wa ghasia za 2015 kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula mwengine wa tatu.
- Burundi yawapiga marufuku wachunguzi wa UN
- Burundi yakataa polisi wa UN
- Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kutoka Tanzania
Utawala wa Burundi unasema kuwa ni salama kwa raia kurudi nyumbani
No comments