Header Ads

Watu 7 wamekamatwa Uganda kwa kupinga kikomo cha umri wa rais

Wanaharakati vijana wa Uganda
Image captionWanaharakati vijana wakiandamana kupinga kikomo cha umri wa rais
Takriban watu saba wametiwa nguvuni katika mji mkuu wa Uganda kampala , kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya muswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais.
Katiba ya sasa inasema kikomo cha umri wa urais ni miaka 75.
Mabadiliko ya katiba yatamruhusu rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021.
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUmri halisi wa rais wa sasa wa Uganda Yoweri Museveni ni miaka 73, kulingana na Wikipedia
Umri halisi wa rais Museveni haufahamiki, lakini mtandao wa Wikipedia unasema ana umri wa miaka 73
Wanaharakati vijana wa kundi lijulikanalo kama-The Alternative, ambao waliandaa maandamano hayo, wanasema ofisi yao ilivamiwa jana na wanajeshi pamoja na polisi.
Wanadai laptop, compyuta pamoja na nyaraka nyingine za kampeni yao vilichukuliwa wakati wa uvamizi huo.

No comments