Header Ads

WANACHUO WAONYWA.






Wanachuo wa chuo cha uandishi wa Habari ( The Arusha East Africa Training Insitute) kilichopo mtaa wa Philips  Arusha  mjini watakiwa kufuata sheria na taratibu za chuo kipindi chote watakapokuwa chuoni. Hayo yamesemwa na Bw.Karia Victor ambaye ni mtaaluma wa chuo hicho alipokuwa akiwaasa  kwenye mdahalo wa wanachuo uliofanyika leo Oktoba 20, 2017 hapo chuoni.
   Mbali na kufuata sheria pia amewataka kila mwanachuo avae sare maalumu ya chuo(T-Tshirt) hasa kwa siku ya Ijumaa ya kila wiki wanapokuwa chuoni.

   Aidha Bw. Karia Victor amewatangazia wanachuo kuwa watakuwa na ziara ya kimasomo siku ya Ijumaa ya oktoba 27, 2017 kituo cha Habari kilichopo Arusha na kuwataka kila mwanachuo wa chuo hicho cha Uandishi wa habari kuwa na vifaa vya taaluma yake siku hiyo.



No comments