Arsene Wenger: Sanchez na Ozil hawaondoki ng'o
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji Alexis Sanchez na kiungo wa kati Mesut Ozil wataichezea Arsenal baada ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari hadi pale ''kitu kisiochoaminika kitakapofanyika''.
Kandarasi ya wachezaji hao wawili inakamilika mwishoni mwa msimu huu.
Alipoulizwa iwapo anahisi watasalia, Wenger alijibu: Ndio kabisa.
Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa Jack Wilshere pia anataka kusalia na klabu hiyo ya ligi ya Uingereza.
Wenger aliongezea: Nitampigania asalie hapa kwa sababu ni mchezaji mzuri.
Mchezaji wa Uingereza Wilshere mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akikumbwa na majeraha tangu alipoingia Arsenal 2008 huku akihudumu msimu wa mwaka 2016-17 kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth.
Hatahivyo hajaanzishwa msimu huu.
Wote, Sanchez mwenye umri wa miaka 28 na Ozil mwenye umri wa miaka 29 ni viungo muhimu wa Wenger.
Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye aliwasili kutoka Barcelona 2014 amefunga mabao 56 katika mechi 113, huku Ozil ambaye ni raia wa Ujerumani akitoa usaidizi wa mabao 45 tangu alipojiunga 2013 ikiwa ni zaidi mchezaji yeyote yule.
No comments