Header Ads

Aungua moto hadi kufariki akiwa kitandani kwake

Image result for bad news

Mtu mmoja alie julikana kwa jina la Aisha Yussuf Mbilinyi mwenye umri wa miaka 36 mkaazi wa Kikwajuni juu amefariki dunia akiwa amelala chumbani kwake baada ya kuungua moto.
akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, amesema tukio hilo lilitokea Novemba 26 mwaka huu saa 4:30 huku chanzo cha tukio hilo likiwa halijajulikana.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha Moto huo.

No comments