Mhasibu Mkuu wa TAKUKURU afikishwa Mahakamani
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Godfrey Gugai, amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, na kusomewa mashtaka 44.
Baadhi ya mashtaka aliyosomewa Godfrey gugai, ni pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha na kudanganya mali anazomiliki.
Siku mbili zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Generali, John Julius Mbungo, alitangaza dau nono la shilingi 10 milioni kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Godfrey Gugai, ambaye hakuwa anajulikana alipo, lakini Novemba 15, alijisalimisha mwenyewe na kuhojiwa na taasisi hiyo.
TAKUKURU imemfikisha mahakamani, Gugai kwa tuhuma za kumiliki mali nyingi ambazo haziendani na kipato chake jambo ambalo ni kunyume cha sheria ya Utumishi wa Umma.
Mali zilizotajwa kumilikiwa na Gugai ni pamoja na viwanja zaidi ya 30, magari matano, nyumba 5 na piki piki moja ambavyo vitu hivyo viko maeneo mbalimbali hapa nchini.
No comments