Header Ads

PICHA 5: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amjulia hali Tundu Lissu Kenya



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Novemba 28, 2017 amemtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayeendelea kupata  matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

 Aidha,Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake ya maendeleo na taifa kwa ujumla.

Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais John Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao ya kila siku.






No comments