Header Ads

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia


Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Songea.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho amethibitisha msiba huo.

“Nimepata taarifa jana usiku (Alhamisi Novemba 23,2017) kuwa Gama amefariki kwa kuugua shinikizo la damu,’’ amesema na kuongeza;
 

“Tunawasiliana na familia ili kujua utaratibu wa mazishi. CCM tunasikitika kwa msiba huu, msiba ni wetu sote.”

Gama enzi za uhai wake amewahi kuwa Mkuu wa wilaya za Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala kabla ya kuwa Mkuu wa mkoa Kilimanjaro
By, Mwananchi

No comments