Header Ads

JAMES MBATIA AVUNJIKA MKONO

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono baada ya kuteleza na kuanguka akitokea hotelini kuelekea nyumbani kwake.
  Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).
   Tukio hilo lilitokea jana saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.Msaidizi wake Hamis Hamis amesema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.
"Huduma za matibabu bado zinaendelea lakini bado maumivu bado ni makali sana" alisema Mbatia

No comments