Header Ads

KENYA YAPIGA MARUFUKU SHISHA




Wateja wakivuta Shisha Khartoum April 28, 2013

Wateja wakivuta Shisha Khartoum April 28, 2013


Wizara ya Afya imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini Kenya.
Katika amri ya serikali iliyochapishwa katika gazette la serikali, Waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, utangazaji na uuzaji wa biashara hiyo ya shisha nchini.
Katika amri ya kisheria iliyotolewa Disemba 28, Dkt Mailu ameonya kuwa mtu yoyote atayekutikana akivunja sheria hiyo ya kupiga marufuku utumiaji wa shisha atatakiwa kulipa faini isiyozidi Shilingi 50,000, au kifungo cha muda usiozidi miezi sita, au adhabu zote mbili.”
Na kama kosa hilo la ukiukaji sheria litaendelea, mkosaji atatozwa faini zaidi isiyozidi Shilingi 1,000 kwa kila siku uvunjifu huo wa sheria ulipoendelea kama itakavyo kuwa imeelezwa katika kifungu 163 cha Sheria ya Afya ya Jamii.
“Hakuna mtu atakaye ingiza, tengeneza, uza au kukiweka sokoni kuuzwa, kutumia, kutangaza, kushawishi, kuwezesha au kuwapa moyo watu kutumia shisha nchini Kenya,” imesema sehemu ya amri hiyo.
Akithibitisha kutolewa kwa tamko hilo la kisheria, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Jackson Kioko amesema: “ Uamuzi wetu wa kupiga marufuku katika kila hali umejiridhisha kutoka pande zote … ikiwa kijamii mpaka afya na imezingatia ushahidi wa vipimo vya kisayansi juu ya athari mbaya za uvutaji shisha.
Katazo hili linaifanya Kenya kuwa nchi ya tatu katika Afrika Mashariki kupiga marufuku shisha baada ya Tanzania na Rwanda.
Nchi nyingine zilizopiga marufuku shisha ni Pakistan, Jordan, Singapore na Saudi Arabia

No comments